Waliopigwa na askari wa TANAPA wapewa milioni 5

0
61

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa ametoa mkono wa pole wa shilingi milioni moja kwa kila mmoja kwa wananchi watano wa kijiji cha Mwanavala wilayani Mbarali mkoani Mbeya kama kifuta machozi kutokana na ugomvi wa wahifadhi na wananchi hao.

Waziri Mchengerwa amefika kijijini hapo kutokana na agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa lililotolewa Mei 11, 2023 bungeni Dodoma kuitaka Wizara ya Maliasili kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Mbeya kutatua migogoro baina ya Hifadhi ya Ruaha na wananchi.

RC Homera atoa saa 24 askari wa TANAPA waliopiga wananchi wakamatwe

Waziri Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wote wa Serikali walioshiriki kwenye migogoro huo.

Akiongea kwenye kikao na wananchi hao, Waziri Mchengerwa amewaomba wananchi kuzingatia sheria na kuwataka kutovamia maeneo ya makazi ambapo amesema katika mgogoro huo baadhi ya wananchi walikutwa kilomita kumi ndani ya hifadhi, ndipo walipoanza kutolewa kwa nguvu na wahifadhi.

Hata hivyo, Mchengerwa amesema imethibitika kuwa madai ya kwamba ng’ombe 250 walishikiliwa siyo ya kweli kwa kuwa wananchi wote katika mkutano wamekubali kuwa hakuna ng’ombe hata moja aliyeshikiliwa na hifadhi.

Send this to a friend