kuokoa watu waliopata ajali ya ndge ya Precision Air Novemba 06, 2022 wameomba nao kupewa mafunzo ya uokozi.
Akisimulia tukio hilo mmoja wa vijana hao amesema baada ya ndege hiyo kuanguka yeye, Majaliwa na wenzake wawili ambao walikuwa mwalo wa Nyamkazi wakiendelea na shughuli zao, walikuwa wa kwanza kufika katika eneo la ajali ili kuwaokoa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Waathirika wa ajali ya Precision Air kulipwa TZS bilioni 396
Wamesema Majaliwa ndiye aliketi eneo la mbele la mtumbwi, wenzake walimpa kasia ili autumie kupiga mlango katika jitihada za kuufungua huku wakishirikia kuuvuta kwa kutumia mkanda ndipo mlango ulipofunguka ghafla na kumbamiza Majaliwa kwenye paki la uso hadi kuzimia na kukimbizwa hospitali sambamba na majeruhi wengine wa ajali ya ndege waliokolewa.
Akijibu swali la kwa nini wao hawakutajwa, huku sifa zote akipewa Majaliwa wakati walishirikiana wote, Sadath amesema hilo limetokana na Majaliwa kujeruhiwa hadi kulazwa wakati wao walisalia eneo la ajali wakiendelea kushirikiana na watu wengine kujaribu kuvuta ndege ili kuokoa watu 19 waliosalia ndani.
Chanzo: Mwananchi