Waliozaliwa na jinsia mbili washauriwa kwenda hospitalini peke yao

0
38

Watanzania waliozaliwa na changamoto ya ulemavu wa kuwa na jinsia mbili wameshauriwa kwenda hospitalini peke yao wanapofikisha umri wa miaka 18 kwa ajili matibabu.

Akizungumza Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Edna Majaliwa amebainisha kuwa wengi waathiriwa na jinsia mbili, wanakwenda hospitalini na wazazi wao wakiwa katika umri mdogo, lakini kitaalamu wanatakiwa kuhudhuria peke yao wanapofikisha miaka 18.

“Tunapendekeza watu wenye ulemavu wa aina hiyo, waje hospitalini peke yao, wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 18, ili kuamua juu ya hali yao ya jinsia,kama watafanyiwa upasuaji ili kubaki mwanaume au mwanamke,” amesema Daktari.

Vigezo 10 vinavyoangaliwa zaidi na wanaume kwa wanawake wanapotaka kuoa

Aidha, Dk Edna amebainisha kuwa waathiriwa wa jinsia mbili wakati wa kujamiiana wanapitia utendaji kazi wa kiungo kimoja cha ngono kuliko kingine, hali inayosababisha kukandamizwa kwa kiungo dhaifu na kuimarisha kimoja chenye nguvu, na ndicho kinaweza kuamua kubaki mwanaume au mwanamke.

Kulingana na utafiti wa Shirika moja Lisilo la Kiserikali (NGO), hadi kufikia mwaka juzi jumla ya waathiriwa nchini walikuwa 37, huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuwa na waathiriwa tisa, ikifuatiwa na Mkoa wa Kagera wenye idadi ya waathiriwa sita.

Chanzo: Raia Mwema.

Send this to a friend