Waliyozungumza Rais Samia na CEO wa Royal Dutch Shell ya Uholanzi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Dutch Shell, Ben Van Beurden ameeleza kuwa wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha mazungumzo ya uwekezaji kwenye mradi wa gesi asili iliyosindikwa (LNG) hapa nchini.
Van Beurden amesema hayo leo wakati wa mazungumzo kwa njia ya mtandao na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Van Beurden kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao utachochea kukuza uchumi wa Tanzania.
Shell yenye makao yake makuu nchini Uholanzi inajihusisha na biashara ya gesi ambapo kwa Tanzania ina ofisi zake kuu jijini Dar es Salaam.