
Marekani imewashitaki raia wake wanne kwa kuhusika kwenye jaribio la kupindua Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya watatu kati yao kurejeshwa mikononi mwa mamlaka za Marekani.
Watatu kati yao; Marcel Malanga, Tyler Thompson, na Benjamin Zalman-Polun walihukumiwa kifo nchini DRC kabla ya hukumu yao kubatilishwa na Rais Felix Tshisekedi na kuwa kifungo cha maisha.
Wamarekani watatu waliohukumiwa kifo DRC warudishwa kwao
Kwa sasa, washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutumia silaha za maangamizi, kulipua majengo ya serikali, na kupanga kuua au kuwateka nyara watu katika nchi ya kigeni.
Watatu hao waliachiliwa huru Jumanne katika makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya mshauri mkuu wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika, Massad Boulos, nchini DRC.