Wamiliki wa TikTok wapinga Marekani kuwalazimisha kuuza programu hiyo

0
45

Baada ya Serikali ya Marekani kuwataka wamiliki wa TikTok kutoka China kuacha hisa zao katika program hiyo au watapigwa marufuku katika soko lake, China imesema itapinga vikali kuuza programu hiyo kwa kulazimishwa.

Maoni hayo yamekuja wakati Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok, Shou Chew akizungumza mbele ya wabunge wa Marekani huku kukiwa na uchunguzi mkubwa juu ya uhusiano wa programu hiyo na Beijing.

Wizara ya biashara ya China imesema kwamba uuzaji wa kulazimishwa wa program hiyo ya TikTok utavunja sana imani ya wawekezaji wa kimataifa kwa Marekani.

Marekani yatishia kupiga marufuku mtandao wa TikTok

“Ikiwa habari [kuhusu mauzo ya kulazimishwa] ni ya kweli, China itaipinga vikali,” Shu Jueting, msemaji wa wizara hiyo wakati akizungumza na wanahabari Alhamisi huko Beijing, na kuongeza kuwa mpango wowote utahitaji idhini kutoka kwa serikali ya China.

Ameeleza kuwa “uuzaji au uondoaji wa TikTok unahusisha usafirishaji wa teknolojia, na taratibu za utoaji leseni za kiutawala lazima zifanywe kwa mujibu wa sheria na kanuni za China. [..] Serikali ya China itafanya uamuzi kwa mujibu wa sheria.”

Send this to a friend