Wamuua dada yao wakigombania zawadi za Krismasi

0
86

Ndugu wawili wamekamatwa mjini Florida baada ya dada yao kupigwa risasi na kuuawa wakati wa mabishano kuhusu zawadi za Krismasi.

Kwa mujibu wa polisi, msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 alipigwa risasi kifuani na kaka yake huku akiwa na mtoto wake wa kiume wa miezi 10 kwenye gari la kubebea mizigo ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo, mhalifu huyo alipigwa risasi na kaka yake mkubwa kupitia bunduki yake mwenyewe.

“Ufyatuaji huo ulifuatia mabishano juu ya nani alikuwa akipokea zawadi zaidi,” imesema taarifa ya polisi.

Taarifa imeeleza kuwa baada ya kijana mkubwa mwenye umri wa miaka 15 kutekeleza tukio hilo alikimbia kutoka eneo la tukio na kutupa bunduki yake ambapo baadaye alikamatwa na kufunguliwa kesi ya kujaribu kuua.

Ndugu mdogo, mwenye umri wa miaka 14, alipelekwa hospitalini akiwa katika hali ya kuridhisha na atawekwa chini ya ulinzi atakapoachiliwa kwa mujibu wa polisi.

Send this to a friend