Waandamanaji Kenya watawanywa kwa mabomu ya machozi

0
55

Polisi wa kutuliza ghasia jijini Nairobi nchini Kenya wamewatawanya waandamanaji na kuwakamata baadhi yao walioandamana kuipinga Serikali ya Rais William Ruto pamoja na kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini humo.

Maandamano hayo yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, yametawanywa kwa mabomu ya machozi ambapo waandamanaji walichoma matairi.

Rais Ruto amesema haoni sababu ya maandamano hayo huku akimshutumu Odinga kuisababishia nchi machafuko.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki pia alitoa taarifa siku ya Jumapili Machi 19, 2023 akionya kwamba yeyote atakayechochea ghasia au kuvuruga amani atachukuliwa hatua.

Send this to a friend