Wanafunzi 1,050 wafutiwa matokeo darasa la saba

0
49

Jumla ya wanafunzi 1,059 kutoka shule 38 wamefutiwa matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2020 araza la kutokana na udanganyifu uliofanyika wakati wa mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi.

Akizungumza wakati akitangaza matokeo ya mitihani hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde amesema watahiniwa hao hawatapata nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo.

Msonde amesema shule hizo zilifanya makosa mbalimbali ikiwamo kuiba mitihani, kuwapa wanafunzi pamoja kuruhusu watahiniwa kufanyiwa mitihani na watahiniwa wasio halali.

Shule ambazo wanafunzi wake wamefutiwa matokeo ni pamoja na Ngiloli, Nguyami, Ibuti, Ihenje, Bwawan, Chakwale, Msingisi zilizopo Halmashauri ya Gairo.

Zingine ni Mafiri, Kibogoji, Ng’wambe, Digalama, Dihinda kutoka Halmashauri ya Mvomero na shule za msingi za Nyawa A iliyopo Halmashauri ya Bariadi vijijini (Simiyu).

Shule zingine ni za Halmashauri ya Chabutwa, Sikonge Tabora ikiwemo shule ya msingi Chabutwa, Usagari, Uyui Tabora Siashimbwe iliyopo Moshi Kilimanjaro, Dominion Arusha, Matogoro ya Tandahimba Mtwara, Ng’arita Bariadi vijijini mkoani Simiyu, Olkitikiti Kiteto iliyopo Manyara na Nyamimina Buchosa Mwanza.

Jumla ya wanafunzi 1,023,950 walifanya mtihani huo mwaka huu. Unaweza kutazama matokeo hayo hapa.

Send this to a friend