Wanafunzi 150,000 wapangiwa kidato cha tano na vyuo

0
45

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mwaka 2022.

Amesema jumla ya wanafunzi 153,219 (wasichana 67,541 na wavulana 85,678), sawa na asilimia 91.8 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu ya ufundi.

Aidha, ameongeza kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano wanatakiwa kuripoti Juni 13 hadi 30, mwaka huu katika shule walizopangiwa huku akisisitiza kwa watakaochelewa kujiunga nafasi zao zitachukuliwa na watu wengine wenye uhitaji.

Hata hivyo, amewasihi wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa mamlaka ya Serikali za mitaa, kuhakikisha azma ya Serikali ya kuwa na shule za sekondari za kidato cha tano katika kila halmashauri inatekelezwa ili wanafunzi wanaofaulu kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

Send this to a friend