Wanafunzi 188,128 wachaguliwa kidato cha tano na vyuo

0
55

Ofisi ya Rais TAMISEMI imesema wanafunzi 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule pamoja na vyuo vya fani mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amesema kati ya hao wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika Shule za sekondari Maalum 8 za Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.

Aidha, Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa katika shule 519 za Sekondari za Bweni za Kitaifa za Kidato cha Tano, huku wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515 na wavulana 2,529 wakipangwa katika shule 11 za sekondari za kutwa za kidato cha tano.

Send this to a friend