Wanafunzi wa Diploma kupewa mikopo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Eliamani Sedoyeka amesema Serikali ilianzisha majadiliano na Benki ya NMB ambayo imekubali kutenga TZS bilioni 200 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wakiwemo wa ngazi ya Stashahada.
Profesa Sedoyeka amesema kwamba hatua hiyo itafungua wigo mpana kwa kundi hilo ambalo halikuwa sehemu ya wanufaika hapo awali, kwa kuwa mkopo ulitolewa kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya shahada pekee.
“Makubaliano ni kwamba NMB watakopesha watu wote na sio tu watumishi wa Serikali au walioajiriwa ili kutoa fursa zaidi na kuongeza wigo wa Watanzania kujiendeleza kielimu zaidi,” amesema.
Aidha, ametoa ufafanuzi kwamba, mkopo huo utatolewa kwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma stashahada kwa sababu wengi wao ni wadogo (chini ya umri wa miaka 18), wakati wale wanaotaka shahada na wanaotaka kujiendeleza kimasomo watakopa wenyewe.