Wanafunzi waliofariki katika ajali Arusha wafikia watano

0
65

Wanafunzi waliofariki kutokana na ajali ya gari la Shule ya Msingi Ghati Memorial ya mkoani Arusha katika mitaa ya Dampo Sinoni, Kata ya Muriet wamefikia watano baada ya miili minne ya wanafunzi kupatikana.

Gari hilo (T496 EFK) lilitumbukia kwenye korongo mapema leo ambapo mpaka sasa wanafunzi watatu, mwalimu na dereva wameokolewa huku zoezi la kuwatafuta wengine likiendelea.

Imeelezwa kuwa dereva wa gari hilo alizuiwa kupita katika sehemu hiyo yenye korongo lakini alisema anaweza kupita kwa kuwa awali alipokuwa akiwapeleka wanafunzi hao aliweza kupita njia hiyo.

Gari hilo lilikuwa na watu 13 wakiwemo wanafunzi 11 na dereva na matroni wa shule hiyo.

Send this to a friend