Wanafunzi wanaovuta bangi wawatishia walimu, waiba nyaraka za wanafunzi wenye makosa

0
73

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyela jijini Mbeya wanadaiwa kuungana na wanafunzi wa shule ny ingine pamoja na vijana wa mitaani kuvuta bangi na kuwatishia usalama waalimu wao.

Mkuu wa shule hiyo, Christopher Kamendu amesema wanafaunzi hao ambao huwa katika sare za shule hutoroka shuleni na kwenda kuvuta mbangi kwenye eneo liitwalo ‘chimbo’.

Aidha, amesema wanafunzi hao hununua bangi kutoka kwa vijana wa mitaani ambao huungana na kufanya vitendo vya uhalifu shuleni ikiwemo kuharibu miundombinu ya shule.

Ameongeza kuwa huwatishia waalimu wao kwa kuwaandikia jumbe mbalimbali kisha kuwatupia kwenye ofisi ya mkuu wa shule na maeneo mengine ambayo wanahisi zitaonekana.

Namna 5 bora za kumlinda mwanao dhidi ya hatari za mitandao ya kijamii

Awali inadaiwa vijana hao kwa kushirikiana na vijana wa mitaani walivunja ofisi ya nidhamu ya shule hiyo na kuiba nyaraka mbalimbali zikiwemo nyaraka zinazohusu makosa yanayowahusu wanafunzi hao.

“Lakini hawa vijana wa mitaani waliingia hapa na kuwachukua baadhi ya wanafunzi na kwenda nao huko chimbo wakaanza kuwapiga na kuwaloweka kwenye maji, na haijulikani sababu iliyofanya wafanye hivyo,” amesema Kamendu.

Naye Ofisa Elimu wa Kata ya Kyela, Julius Mgala amesema baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao hawatoi ushirikiano kwa waalimu kudhibiti nidhamu za watoto, hali inayochochea zaidi vitendo vya uhalifu.

Chanzo: Nipashe.

Send this to a friend