Wanafunzi wanne wafariki baada ya kugongwa na gari wakivuka barabara

0
40

Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Afisa Ardhi wa Wilaya ya Nyag’hwale mkoani Geita, Agostino Sibeye kwa tuhuma ya kuwagonga na na kusababisha vifo vya gari Wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Ibambila iliyopo Kata ya Kharumwa.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi wakati wanafunzi hao wakivuka barabara kuelekea shuleni ambapo wote walifariki papo hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba wanamshikilia afisa huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier yenye usajili wa namba T186 DPR.

Kamanda Mwaibambe amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, kwani eneo hilo lina shule na waendesha magari hutakiwa kwenda taratibu.

Send this to a friend