Wanafunzi wasombwa na maji wakiogelea mtoni

0
49

Wanafunzi wawili wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Tumaini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia kwa kusombwa na maji wakati wakiogelea Mto Karanga.

Kamanda wa Jeshil la Zimamoto na Uokoai mkoani humo, Jeremiah Mkomagi amesema tukio hilo limetokea Januari 27, mwaka huu wakati watoto hao ambao ni Lodrick Orota (14) na Ridhiwan Kimath (13) walipotoka shule na kwenda kuogelea mtoni.

Ameongeza kuwa mwili wa Rodrick ulionekana Januari 30 baada ya kukaa kwenye maji kwa siku tatu, huku jitihada za kuutafuta mwili wa Ridhiwani zikiendelea kufanywa na Jeshi hilo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend