Wanafunzi zaidi ya 100 waumwa baada ya kula chakula chenye nyoka aliyekufa

0
5

Shirika la Haki za Binadamu nchini India linachunguza tukio la zaidi ya watoto 100 kuumwa baada ya kula chakula cha mchana shuleni ambacho kilidaiwa kuwa kilikuwa na nyoka aliyekufa.

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Mokama, jimbo la Bihar mashariki mwa India, ambapo inadaiwa mpishi aliondoa nyoka huyo kutoka kwenye sufuria lakini bado akagawa chakula hicho kwa wanafunzi takriban 500.

Baada ya wanafunzi hao kuanza kuumwa, wananchi wa eneo hilo walifunga barabara na kufanya maandamano.

Tukio kama hilo limewahi kutokea mnamo mwaka 2013, ambapo chakula kilichokuwa na sumu kilisababisha vifo vya watoto 23 wa shule katika jimbo hilo la Bihar na uchunguzi ulibaini viwango vya juu vya sumu vilipatikana.

Send this to a friend