Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia utoaji kiasi cha shilingi bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000 vitakavyoweza kupokea wanafunzi wa ziada wa kidato cha kwanza 400,000 ambao ni zao la Elimumsingi bila ada.
Hayo yamesemwa na Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari, 2023.
Amesema kwa sasa fedha hizo zimeshatumwa na kupokelewa kwenye Halmashauri zote 184, kulingana na upungufu uliowasilishwa na kila Halmashauri husika.
Watumishi wanne wafukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha
Bashungwa amefafanua kuwa kwa mwaka 2023, takribani wanafunzi 1,148,512 wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza ambao ni wale walioanza darasa la kwanza mwaka 2016, kipindi ambacho Serikali ilianza utekelezaji sera ya Elimumsingi bila ada Desemba, 2015.
Aidha, amesema matarajio ni kuwa nafasi zilizopo kwa ajili ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza zitokane na uwepo wa shule mpya za Sekondari, ujenzi wa miundombinu mipya na nafasi zilizoachwa na wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne.