Timu ya Waandishi wa habari na watumishi wa Serikali wamejeruhiwa na vijana zaidi ya 200 wa jamii ya Kimasai (Morani) jioni ya Agosti 15, mwaka huu katika eneo la Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha.
Watumishi hao wamekuwa wilayani humo wakiwa katika jukumu la utoaji elimu kwa wananchi waliojitokeza kujiandikisha kuhama kwa hiari katika Kijiji cha Endulen kilichopo ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Wakati zoezi hilo likiendelea, vijana wa Kimaasai wakiwa na silaha mbalimbali za jadi yakiwemo mapanga, sime na mikuki waliwavamia na kuwashambulia kwa silaha hizo wanahabari na watumishi hao.
Wote waliojeruhiwa katika tukio hilo wamefikishwa hospitali iliyopo Karatu kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya dharura.
Mamlaka ya Hifadh ya Ngorongoro imesema inashirikiana na Jeshi la Polisi kuwasaka wote waliohusika katika tukio hilo ili hatua za kisheria zichukuli