Wanahabari sita wakamatwa Sudan Kusini kwa kusambaza video ya Rais Kiir

0
43

Wanahabari sita wa Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) wanashikiliwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo kutokana na kuonesha picha za Rais wa nchi hiyo akionekana kutokwa na haja ndogo.

Waandishi hao wanatajwa kuwa Joval Tombe, Victor Lado, Joseph Oliver, Jacob Benjamin, Mustafa Osman, na Cherbek Ruben

Video hiyo iliyorekodiwa wakati wa hafla, inamuonesha Rais Salva Kiir akisimama kwa ajili ya wimbo wa taifa ambapo anaonekana kutokwa na haja ndogo kisha kamera inaondolewa ghafla baada ya Rais na timu yake kuonekana kutambua kinachoendelea.

Hata hivyo inaelezwa kuwa wanahabari hao wanadaiwa kuvujisha video hiyo Desemba 22, 2022 na kusambaa mitandaoni licha ya kuwa haikuonekana kwenye chaneli za SSBC.

Naye mwakilishi wa Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ), Muthoki Mumo amesema mamlaka inafaa kuwaachilia bila masharti wafanyakazi hao na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bila vitisho vya kukamatwa.

Send this to a friend