Wanajeshi 17 wauawa katika mapigano nchini Niger

0
58

Wizara ya Ulinzi nchini Niger imesema takribani wanajeshi 17 wamefariki na wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulio la wanamgambo wa Kiislamu nchini humo.

Taarifa ya wizara imesema shambulio hilo la ghafla limetokea katika eneo la Tillabéri, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.

Hata hivyo taarifa imeeleza kuwa wanamgambo zaidi ya 100 wameuawa na wanajeshi wa Niger katika mapigano hayo.

Tukio hilo linakuja wiki tatu baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, huku viongozi wakisema walichukua hatua baada ya serikali iliyochaguliwa kutochukua hatua kudhibiti ghasia za jihadi.

Vikosi vya jeshi vya Niger vimeeleza kuwa kuenea kwa uasi wa wanamgambo wa jihadi ni moja ya sababu zilizopelekea mapinduzi ya kijeshi.

Send this to a friend