Wanajeshi wa Israel watekwa, Marekani yaahidi kusimama na Israel

0
69

Israel na Hamas kwa mara nyingine tena wako vitani baada ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina kuanzisha operesheni kubwa ya anga na ardhini leo asubuhi kutoka ukanda wa Gaza.

Zaidi ya makombora 5,000 yamerushwa kutoka Gaza kuelekea Israel, na watu wenye silaha wa Hamas waliingia katika miji na vijiji vingi vya Israel vya pembezoni kwa mujibu wa jeshi la Israel ambapo Israel pia imejibu mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza na mapigano bado yanaendelea kusini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Israel lilithibitisha kuwa raia na wanajeshi bila kutaja idadi yao, wamechukuliwa mateka na sasa wako Gaza. Vyombo vya habari vya ndani vinakadiria kuwa makumi ya wanajeshi wameshikiliwa.

Naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Saleh al-Arouri ameeleza wazi kwamba maafisa wakuu wa jeshi la Israel wamekamatwa.

Aliiambia Al Jazeera kwamba “kile kilicho mikononi mwetu kitawaacha huru wafungwa wote” nchini Israel ikiwa ni kumbukumbu ya Wapalestina wanaozuiliwa katika magereza za Israel.

Makundi ya Wapalestina siku za nyuma yamekuwa yakiwatumia mateka kama njia ya mazungumzo ili kuhakikisha wanamgambo wanaoshikiliwa na Israel wanaachiliwa, na kwa mujibu wa taarifa, Israel inawashikillia Wapalestina 4,499 gerezani.

Idadi ya vifo nchini Israel inakadiriwa kuwa 100, na takriban watu 1000 wamejeruhiwa, kulingana na huduma za dharura za Israeli huku idadi ya vifo katika ukanda wa Gaza imeongezeka hadi 198 na watu 1,610 wakijeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya Palestina.

Kwa mujibu wa taarifa ya CNN, Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizunguma leo kwa simu na kumhakikishia kwamba Marekani inasimama upande wa Israel na inaiunga mkono katika kujilinda dhidi ya mashambulizi.

Send this to a friend