Wanajeshi watatu wa Tanzania wajeruhiwa DR Congo

0
47

Wanajeshi watatu wa Tanzania ambao ni sehemu ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejeruhiwa katika mapigano na wanamgambo wa M23.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa tayari wamepelekewa katika mji wa Goma kwa ajili ya matibabu baada ya kujeruhiwa huko Rutshuru, Jimbo la Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la DR Congo, mmoja wa wanajeshi hao amejeruhiwa vibaya zaidi.

Tanzania ina zaidi ya wanajeshi 800 nchini humo. M23 imelituhumu jeshi la nchi hiyo na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuwa wamechagua vita badala ya mazungumzo.

Chanzo: BBC

Send this to a friend