Wanakijiji wamchangia kiwanja muuguzi kwa kuwahudumia kwa upendo

0
95

Wananchi wa Kijiji cha Ngomai Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wamechanga zaidi ya TZS milioni 4 kwa ajili ya kumnunulia muuguzi wa kijiji hicho, Peter Mwakalosi kiwanja kwa kufanya kazi kwa moyo na upendo na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Wanakijiji hao wamesema wameamua kuchanga pesa kwa ajili ya kiwanja cha muuguzi huyo ili ajenge nyumba na kuishi hapo hata baada ya kustaafu kazi.

Akizungumza Diwani wa Kata ya Ngomai, Mfaume Mlimila amemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo asimhamishe muuguzi huyo kijijini hapo kwani wanakijiji wanampenda kwa utendaji wake mzuri.

Mlimila amesema muuguzi huyo amefanikiwa kuondoa dhana potofu ya wananchi kutibiwa kwa waganga wa kienyeji magonjwa ambayo hapo awali hawakuamini yanaweza kutibika katika hospitalini hiyo tangu alipofika kijijini hapo mwaka 2005.

Send this to a friend