Wanakijiji wamzika ndani ya nyumba yake mwanaume wanayedai ameuawa na ndugu zake

0
59

Wakaazi wa kijiji cha Gesabakwa eneo la Bomachoge Borabu kaunti ya Kisii nchini Kenya wamemzika mwanaume aliyeuawa na watu wasiojulikana ndani ya nyumba yake kabla ya kuwatimua familia yake kwa madai ya kuhusika na tukio hilo.

Marube, ambaye mwili wake ulikutwa kwenye chumba chake cha kulala baada ya kupigwa na kitu butu, alizikwa ndani ya sebule ya nyumba yake baada ya wazee wa kijiji kufanya ibada maalum kabla ya kuchimba kaburi.

Wanakijiji waliokuwa na hasira wamesema kifo cha Marube ni cha kutatanisha na hakuna mashaka kuwa familia yake inahusika katika kumfanyia ukatili huo.

Wiki moja kabla ya mazishi hayo, wakazi wa kijiji hicho walitembea kilomita 10 hadi Kituo cha Polisi cha Kenyenya wakidai majibu kuhusu mazingira ya kifo cha Marube na vifo vya watu wengine kumi ambao wameuawa kwa njia za kutatanisha katika miaka ya hivi karibuni.

Send this to a friend