Wanakwaya wafariki katika ajali Njombe

0
75

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amethibitisha kutokea vifo vya watu watatu kutokana na ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Toyota Coaster na lori lililobeba makaa ya mawe usiku wa kuamkia leo katika eneo la Igima, wilayani Wanging’ombe Mkoa wa Njombe.

Kwa mujibu wa taarifa, miongoni mwa watu waliofariki ni pamoja na waimbaji wa kwaya ya vijana wa Kanisa katoliki Mkoa wa Njombe (UVIKANJO) waliokuwa njiani wakienda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila wilayani humo.

“Ni kweli tukio hili limetokea kwa sasa tupo huku maporini bado tunaendelea na uokoaji, mvua ni kubwa na kazi ni ngumu, taarifa kamili tutaitoa baadaye,” amesema Kamanda Issah

Hata hivyo habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kuna idadi kubwa ya majeruhi.

Send this to a friend