Wananchi Kenya wajitokeza kuuza figo

0
43

Hospitali Taifa nchini Kenya imesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaouliza na kujitolea kuuza figo zao.

Katika chapisho la Facebook, hospitali hiyo imesema watu wengi wanauliza kupitia ukurasa wao gharama za kutoa figo zao ili kujipatia kipato na kumudu gharama za maisha zilizopanda hivi karibuni.

Aidha, hospitali hiyo imeshauri kwamba, ingawa viungo vya mwili vinaweza kutolewa kwa hiari ya mtu ili kusaidia wenye uhitaji, lakini haviwezi kuuzwa.

“Tafadhali kumbuka kuwa uuzaji wa viungo ni marufuku kabisa na ni kinyume cha sheria. Unaweza tu kuchangia kwa hiari yako,” imesema.

Benki ya Dunia mapema mwezi huu illitaarifu kuwa Afrika Mashariki ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na anguko la uchumi kwa sababu ya vita vya Urusi nchini Ukraine na Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19).

Send this to a friend