Wananchi Moshi waiba mita za maji na kuziuza nje ya nchi

0
57

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Abbas Kayanda, amewaonya  baadhi ya wananchi wanaoiba mita za maji na kuziuza  nchi jirani.

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lole, Kata ya Mwika Kaskazini na kusema kuwa Serikali haitowafumbia macho wale wote wanaofanya uhalifu huo.

“Kumekuwepo na wizi wa mita za maji, na taarifa tulizonazo mnazipeleka nchi jirani kuuza, sasa tunatangaza operesheni kali kuhakikisha wale wote wanaofanya hivi wanakamatwa kisha kufikishwa mahakamani,” amesema.

Mwanafunzi awadanganya wazazi wake ametekwa ili wamtumie fedha

Kayanda ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWASA) kuacha kuweka mita za maji mbali na makazi ya wananchi anayepatiwa huduma hiyo badala yake wazifunge jirani na nyumba.

“Mita ikiibiwa mwanachi hajui kwani ipo mbali na makazi yake, badilikeni, mita hizi mzifunge jirani kabisa na nyumba ya mteja ili aweze kuilinda mwenyewe,” ameeleza.

Send this to a friend