Wananchi wajitolea kumchangia Wakili Madeleka kusimamia kesi ya anayetajwa kuwa ‘Afande’

0
107

Baadhi ya wananchi wamejitolea kumchangia pesa Wakili Peter Madeleka na wenzake kusikiliza kesi dhidi ya SSP Fatuma Kigondo ambaye anatuhumiwa kutuma vijana kumfanyia ukatili binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Duvya Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) amesema kesi hiyo iliyofunguliwa Agosti 20, mwaka huu na Wakili Paul Kisambo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, inatarajiwa kusikilizwa leo na kuwaomba Watanzania wachangie gharama za usafiri wa mawakili watakaokwenda kusimamia kesi hiyo kwa upande unaoshtaki.

“Kwa sababu ya kukosa fedha kuna uwezekano mkubwa kesho nitashindwa kwenda Dodoma kwa ajili ya kesi ya jinai inayomkabili ASP Fatuma Kigondo ngoja tuendelee kumwomba Mungu,” ameandika.

Ujumbe huo uliibua hisia za watu wengi ambapo waliomba namba kwa ajili ya kufanya miamala na wengine wakionesha risiti zao kuthibitisha kuwa wametoa michango yao.

 

Chanzo: Nipashe