Wananchi wawaua kwa mishale maofisa wawili wa Uhamiaji

0
24

Maofisa wawili wa Idara ya Uhamiaji kutoka Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wameuawa kwa kupigwa mishale na wananchi wa kijiji cha Mtakuja Kata ya Lulembela Wilaya ya Mbogwe baada ya kuhisiwa kuwa ni majambazi.

Maofisa hao waliofahamika kwa jina la Salum na Mtobi wameuawa usiku wa kuamkia leo Jumatano Oktoba 26, 2022.

Inadaiwa kuwa maofisa hao waliuawa baada ya kufika kijijini hapo kwa lengo la kuwakamata watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu ambao walikuwa nyumbani kwa mkazi wa kijiji hicho.

Serikali yapiga marufuku mabonanza Shinyanga

Akizungumza na Mwananchi Diwani wa kata ya Lulembela, Deus Lyankando amesema kuwa maofisa hao walishambuliwa na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa ni majambazi kutokana na kitendo chao cha kuvamia na kuvunja mlango wa nyumba ya mzee Masara Lubadili usiku bila kuambatana na kiongozi yeyote wa kijiji wala kata.

“Baada ya mlango kuvunjwa, waliokuwepo nyumbani kwa mzee Masara Lubadili walihisi wamevamiwa na majambazi na hivyo kupiga yowe kuomba msaada ndipo wananchi walipojitokeza na kuwashambulia maofisa hao,” amesema Diwani.

Send this to a friend