Wanao-post vitu vya anasa mitandaoni kuchunguzwa na mamlaka ya mapato

0
42

Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) inawafuatilia watu wanaochapisha vitu vya anasa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwabaini watu wanaokwepa kodi.

Mchapisho yanayoonesha magari ya anasa, majumba ya kifahari, na sherehe (parties) wanafuatiliwa na maafisa wa KRA, amesema Kamishna Mkuu, Githii Mburu.

Mamlaka imesema yeyote atakayebainika kukwepa kodi atakuwa hatarini kuzuiwa kusafiri,  fedha zao kutaifishwa benki ili kulipa madeni yao pamoja na kushtakiwa.

Jitihada hizo za KRA zinalenga kuhakikisha watu wengi zaidi wanalipa kodi, na kudhibiti ukwepaji kodi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kufikia malengo ya makusanyo.

Send this to a friend