Wanaoanza kunywa pombe chini ya miaka 15 hatarini kuwa waraibu

0
42

Utafiti umeonesha kuwa vijana wanaoanza kunywa pombe kabla ya umri wa miaka 15 wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata matatizo ya utegemezi wa pombe pamoja na matatizo ya kiafya tofauti na wanaoanza kunywa pombe baada ya umri wa miaka 21.

Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Kampuni ya Serengeti (SBL), Rispa Hatibu amesema katika utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya mwaka 2008 kwa wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, asilimia 5 ya wanafunzi hao waligundulika kutumia pombe.

Amebainisha kuwa asilimia 10.8 walitumia kabla ya kufikia umri wa miaka 14 na asilimia 26.2 walikuwa na mzazi aliyekuwa anatumia pombe.

Biashara 5 unazoweza kuanzisha kwa mtaji wa TZS 50,000

“Matumizi ya pombe wakati wa utoto na ujana yanaweza kuwa na athari mbaya za kiafya, kijamii, kiuchumi na kimaendeleo kwa vijana na jamii,” amesema Hatibu.

Send this to a friend