Wanaodaiwa kujifanya wafanyabiashara wa madini wakamatwa

0
38

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aboubakar Hamis amesema Jeshi la Polisi linawashikilia watu sita wanaojihusisha na vitendo vya utapeli katika maeneo mbalimbali Zanzibar na Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema watu hao wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa kutumia mbinu kwamba wao ni wafanyabiashara wa madini na kuwashawishi kufanya nao biashara kisha kuwatapeli fedha.

Taarifa ya Aboubakar imeeleza kuwa Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na gari lenye namba za usajili Z 835 KB ambalo linadaiwa kutumika katika utekelezaji wa vitendo hivyo vya utapel

Send this to a friend