Wanaoishi na VVU washauriwa kuacha ngono zembe

0
71

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kutoacha kutumia dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo (ARVs) na kuepukana na vitendo vya ngono zembe.

Akizungumza na wananchi katika kituo cha afya cha Disunyara Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha katika ziara yake ya ya siku moja, Waziri Ummy amesema kumekuwa na kusuasua kwa matumizi ya dawa za ARVs kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi jambo ambalo ni la hatari.

“Katika watu 100 Tanzania wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi 95 wanatumia dawa, tumeona kusuasua kwa matumizi ya ARV kwasababu watu wanaona hawaumwi kwahiyo wanaacha kutumia dawa,” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza, “wakati tunakaribia kuushinda Ukimwi tunaanza kurudi nyuma, hata kama huumwi unaona vimepungua tusiache kutumia dawa na kurudi kwenye ngono zembe.”

Send this to a friend