Wanaosambaza taarifa za vifo mitandaoni kushughulikiwa

0
10

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba ameviagiza vyombo husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote wanaozua taharuki kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu afya za watu wengine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dkt. Nchemba amesema wakati taifa likiwa kwenye majonzi ya kupoteza viongozi wake kumetokea tabia mbaya ya kuzushiana ugonjwa na vifo, jambo ambalo amesema ni kukosa utu, kuathiri maisha bibafsi ya mtu na kusababisha taharuki kwa familia yake.

“Nimeelekeza vyombo vyote husika kuchukua hatua bila kusubiri mtu binafsi akalalamike,” imeeleza sehemu ya chapisho lake.

Ameongeza kuwa kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao kinazuia watu kutoa taarifa za uongo.

“Nani amekupa kazi ya kufuatilia afya za wengine na kuwa msemaji wa hali zao?” amehoji kwenye taarifa yake akitaka wananchi kuacha tabia hiyo haraka.

Send this to a friend