Wanasayansi wafufua moyo wa nguruwe uliosimama dakika 60 baada ya kuchinjwa

0
68

Wanasayansi nchini Marekani wamesema wameweza kufufua viungo vya nguruwe ikiwa ni pamoja na kurejesha mzunguko wa damu katika moyo uliosimama kwa saa moja baada ya wanyama hao kuchinjwa kwa kutumia teknolojia mpya ambayo husaidia kusambaza oxygen.

Dakika 60 baada ya kusimamisha mioyo ya nguruwe hao, watafiti kutokea chuo kikuu cha Yale nchini Marekani waliweza kuanzisha upya mzunguko wa damu katika mioyo hiyo kwa kutumia mashine maalumu.

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia, wanasayansi wamesema kutokana na majaribio hayo ya awali katika nguruwe, zoezi hilo linaweza kusaidia kuongeza idadi ya viungo vinavyopatikana kwa ajili ya upandikizaji na kuokoa maisha ikiwa vitatumika kwa binadamu.

Send this to a friend