Wanaume wa Kinondoni waongoza kwa mabusha

0
48

Wanaume 127 kati ya 165 waliofanyiwa uchunguzi mkoani Dar es Salaam kuanzia Januari 05 hadi 08, mwaka huu, wamepatikana na ugonjwa wa mabusha na

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea hali ya matibabu ya mabusha yanayotolewa bure katika wilaya zote za mkoa huo kuanzia Januari 5 hadi 30 mwaka huu, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mohamed Mang’una amesema tayari wagonjwa 27 wamefanyiwa upasuaji na kwa sasa wanaendelea vizuri.

Aidha, Dkt. Mang’una ameeleza kuwa katika uchunguzi uliofanyika hadi sasa, Wilaya ya Kinondoni imeonekana kuongoza kwa ugonjwa huo.

Dkt. Mang’una amesema kwa sasa ugonjwa huo upo zaidi mikoa ya ukanda wa Pwani kuanzia mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam.

Send this to a friend