Wanaume walalamika wake zao kutowashirikisha fedha wanazopata kwenye VICOBA

0
21

Vikundi vya Kuweka Akiba na Kukopeshana (VICOBA) vimedaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake kutokana na wanawake wengi kuendesha vikundi hivyo kwa kutegemea uchumi wa familia.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa Saikolojia Mkoa wa Mbeya, Sylvester Mwashiuya ambaye ameeleza kuwa wanawake wanaoingia kwenye VICOBA wanategemea fedha zinazotoka kwenye miradi ya familia kuendesha vikundi hivyo hali inayoibua migogoro na kupelekea kufanyiwa ukatili ikiwemo vipigo.

Mkuu wa Polisi Nigeria ahukumiwa kwenda jela miezi mitatu

Mwashiuya amefafanua kuwa kutokana na malimbikizo ya madeni, wahusika hupata msongo wa mawazo na kusahau jukumu la kuhudumia familia hali inayoibua mgogoro ndani ya familia huku wanaume wakilalamika kuwa wanatumia fedha zao lakini unapofika wakati wa kupata fedha hawashirikishwi kwenye fedha hizo.

“Wanaume wengi wanadai kutonufaika na fedha za VICOBA vinavyochezwa na wake zao kwa sababu ni wabinafsi, wanazitumia fedha hizo kufanya maendeleo yao binafsi na si kwa ajili ya ujenzi wa familia,” amesema.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend