Wanaume wanaotafuta ‘six pack’ watahadharishwa kuota matiti

0
71

Wataalamu wa afya nchini wamewaonya wanaume wanaotumia dawa mbalimbali (supplement) kujenga au kukuza mwili ‘six pack’ ili kupata mvuto wa kimaumbile.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya utumiaji wa dawa hizo za ziada huleta athari kwenye homoni inayoweza kusababisha mtumiaji kupata saratani, kupoteza hamu ya tendo la ndoa, kisukari na kukosa nguvu ya kiume.

Matumizi ya dawa hizo hutengeneza ‘six pack’ pia wataalamu wanasema dawa hizo zinaweza kuwa chanzo cha ugumba, madhara kwenye mishipa ya fahamu, kuota maziwa kwa wanaume, matatizo ya kisaikolojia, moyo na shinikizo la damu.

Sababu ya mtu kukoroma anapolala usiku, na namna ya kuepuka

Mtaalamu kutoka kitengo cha Mafunzo na Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) , Dk Pedro Pallangyo ameonya uongezaji wa mwili kwa dawa za aina yoyote kwa sababu hulazimisha ukuaji usio asili wa mwili ambao husababisha pande mbili za mwili kutofautiana ukubwa.

“Jambo la hatari zaidi ni yale maeneo yanayoongezeka seli, zile haziwi na afya inayopaswa na zinakosa sifa ya kuwa kwenye mwili wa binadamu, hivyo mtu anajiweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya misuli,” amesema.

Chanzo: Mwananchi.

Send this to a friend