Wanaume waongoza kwa vifo vya ajali barabarani

0
39

Serikali imesema katika kipindi cha Januari Mosi hadi Desemba 13, mwaka huu jumla ya ajali 1,641 zimetokea barabarani na kusababisha vifo vya watu 1,550 huku wanaume wakiwa 1,189, ambao ni sawa na asilimia 76.7.

Aidha, katika majeruhi 2,562 wa ajali hizo, wanaume waliojeruhiwa ni 1,721 sawa na asilimia 67 huku idadi ya majeruhi wanawake wakiwa 841, ambao ni sawa na asilimia 33.

Makamba: Mtanzania Joshua Mollel aliuawa na Hamas

Akibainisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema madereva 1,226 walifikishwa mahakamani na madereva 2,596 walifungiwa leseni kutokana na makosa mbalimbali.

Send this to a friend