Wanaume washauriwa kupima saratani ya matiti

0
44

Wataalam wa magonjwa ya Saratani mkoani Mwanza wamewashauri wanaume kuwa na utaratibu wa kupima ugonjwa wa saratani ya matiti pale wanapohisi kuwa na maumivu au uvimbe katika matiti yao.

Wataalam wameeleza kuwa ugonjwa huo unaweza kuwapata watu wa jinsia zote mbili hivyo wanaume wametakiwa kwenda kupima ili kujua afya zao.

Sababu 8 zinazosababisha kukosa hamu ya kula

Hayo yamebainishwa na Dkt. Ikupa Mwakapala wa Kitengo cha Saratani kutoka Hospitali ya Rufani Bugando katika maadhimisho ya mwezi wa kuhamasisha uelewa kuhusu saratani ya matiti duniani.

“Ugonjwa huu ni hatari kwa sasa na unaambukizwa kwa watu wa jinsia zote wenye umri wa mtu mzima na unatibika endapo mtu atawahi kupima kabla ugonjwa huu haujafikia hatua ya nne ambayo hauwezi kutibika kabisa,” amesema.

Send this to a friend