Wanaume washauriwa kusimamia wake zao wanyonyeshe

0
67

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Huduma na Lishe wa Wizara ya Afya, Dk Grace Mosha amewataka wanaume kuwashauri na kuwasimamia wake zao kuwanyonyesha watoto ipasavyo ili kuondokana na udumavu wa akili.

Amefafanua kuwa, wakati mwingine wanawake wanashindwa kuwanyonyesha ipasavyo watoto ili matiti yao yasilale kuwafurahisha waume zao jambo linalosababisha udumavu kwa watoto.

“Hata wale ambao wananyonyesha na kujikuta tayari wamebeba mimba nyingine hawapaswi kuwaachisha kunyonya watoto, wanatakiwa kuhakikisha mtoto ananyonya hadi umri unaostahili kuachishwa, nyonyesha tu hata mimba ikifika miezi tisa angalau utakuwa umemsogeza huyu kwenye umri ambao anastahili kuliko kumkatisha,” amesema.

Send this to a friend