Wanawake Geita walalamika kuingiliwa kimwili na Popobawa usiku (video)

0
64

Wakazi wa Kijiji cha Bugando, Kata ya Nzera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita mkoani Geita wamelalamika kuingiliwa kimwili nyakati za usiku na watu wasiojulikana maarufu kama Popobawa hali iliyoibua taharuki kijijini hapo.

Wananchi hao wamelalamika kufanyiwa vitendo hivo nyakati za usiku wakiwa majumbani wamelala ambapo watu wanaodhaniwa kuwa popobawa huingia ndani bila ridhaa ya wahusika.

Waathirika hao ambao ni wanawake wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwani ni hatari kwa afya zao kutokana na watu wanaowaingilia kimwili huku wakiwa hawajui afya yao .

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya wanawake kuingiliwa kimwili usiku, na kwamba serikali imeanza kulifatilia kwa kina suala hilo kwa lengo la kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo hivyo na watakapobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Send this to a friend