Wanawake nchini waongoza kuugua saratani kwa 70%

0
42

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Dkt. Julius Mwaiselenge amesema ugonjwa wa saratani nchini unaendelea kuongezeka kwa kasi huku wanawake wakiongoza kuugua kwa asilimia 70.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwaiselage amesema saratani inayoongoza kwa sasa ni ya mlango wa kizazi ikichukua asilimia 35 ikifuatiwa na ya matiti asilimia 15.

“Unaweza kuona wanawake ndio waathirika zaidi kuliko makundi mengine yoyote kwa sababu hizo zote mbili waathirika ni wanawake,” amesema Dkt. Mwaiselage.

Fahamu madhara yanayotokana na kunywa maji kupita kiasi

Ameendelea kusema kuwa “saratani inaongezeka sana nchini hivyo ningependa kuwaasa wananchi wafike kuchunguza afya zao mapema kwa sababu ikigundulika mapema inatibika na kupona.”

Aidha, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za saratani nchini ambazo zimesambaa katika hospitali zote za kanda “lakini hapa Ocean Road kwa sasa tuna mashine za kisasa za tiba za uchunguzi na upatikanaji wa dawa ni asilimia 100.

Send this to a friend