Wanawake wabakwa wakienda kutafuta maji

0
57

Baadhi ya wanawake na wasichana kutoka katika kata ya Lyamidati, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamedaiwa kukumbana na vitendo vya unajisi na ubakaji pindi wanapokwenda kutafuta maji

Vitendo hivyo vimedaiwa kufanywa na baadhi ya wanaume wakati wanawake hao wakitembea umbali wa zaidi ya kilometa 15 kutafuta maji katika kata ya jirani ya Lyabukande.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tanganyika Senta, Ramadhan Juma amesema licha ya ukatili huo kufanyika dhidi yao wengi wao hushindwa kutoa taarifa kutokana na kutishiwa kurogwa baada ya kufanyiwa ukatili huo.

Ameeleza kuwa “watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia nafasi kufanya vitendo hivyo pindi baiskeli wanazozitumia kusafirisha madumu yenye maji, zinapoharibika njiani, huwavamia na kuwafanyia ukatili.”

Send this to a friend