Wanawake waongoza kuugua maradhi ya moyo

0
44

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema katika kipindi cha siku 39 kuanzia mwaka wa fedha 2022/23, imetoa huduma kwa wagonjwa 11,242 wanawake wakiwa 6,458.

Ameyabainisha hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Prof. Mohammed Janabi wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za JKCI na mwelekeo wake kwa mwaka huu wa fedha.

Unafahamu kuwa parachichi linaweza kukukinga dhidi ya saratani?

Prof. Janabi amesema JKCI katika kipindi cha Julai hadi Agosti 8 mwaka huu, wamehudumia idadi hiyo huku watu wazima wakiwa ni 9,642 na watoto ni 1,600.

“Kati ya 11,242 wanaume ni 4,784 na wanawake ni 6,458. Kliniki zetu zilitoa huduma kwa wagonjwa 10,926 na kulaza wagonjwa 316 ambapo kati yao watu wazima ni 267 na watoto ni 49 huku wagonjwa watatu wakipoteza maisha.” ameeleza.

Send this to a friend