Wanne wakamatwa Arusha kwa kusafirisha punda nje ya nchi

0
45

Jeshi la Polisi Kikiosi cha Kupambana na Kuzuia Wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Longido mkoani Arusha limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne pamoja na mifugo aina ya punda 46 waliokuwa wakisafirishwa nje ya nchi kinyume na taratibu.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia Wizi wa Mifugo nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Simon Pasua amesema watuhumiwa hao ambao kwa sasa majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kipelelezi watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Kamanda Pasua ameongeza kuwa tayari serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilishatoa maelekezo juu ya katazo la kusafirisha punda na mazao yake kutokana na kupungua kwa idadi ya punda huku akiweka wazi kuwa Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote watakao bainika kuhusika na usafirishaji wa punda nje ya nchi.

“Wananchi wote wazingatie sheria namba 17 ya 2003 ya magonjwa ya wanyama ambayo inataka kila mtu anayesafirisha mazao ya wanyama pamoja na mifugo yenyewe kwenda nje ya nchi kuwa na vibali maalum kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,” amesema.

Send this to a friend