Wapenzi wachapwa viboko hadharani baada ya video ya ngono kuvuja

0
60

Polisi nchini Ghana imewakamata washukiwa watatu kwa kosa la kuwachapa viboko hadharani wapenzi kwa madai ya mkanda ya ngono kuvuja na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Video ya kuchapwa viboko imesambazwa ikiwaonesha wapenzi hao waliofungwa kwenye nguzo wakichapwa viboko katika kasri ya Chifu wa kimila, Jumanne alasiri.

Aidha, taarifa ya msemaji wa Chifu imenukuliwa akisema kuwa wakati kitendo hicho kikitendeka Chifu hakuwepo Ikulu, na kuongeza kuwa Chifu analaani kitendo hicho cha kinyama.

Hata hivyo, Polisi wanasema washukiwa hao walikamatwa kwa msaada wa Chifu na baadhi ya wanajamii, na kwamba wanawasaka washukiwa waliosalia ili kuwakamata kuwafikisha mbele ya sheria.

Kuchapwa viboko ni aina ya adhabu inayotolewa na wazee wa kimila katika eneo hilo kwa utovu wa nidhamu japo kuwa haijaidhinishwa na sheria.

Send this to a friend