Wapenzi wengi chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume

0
92

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Tulitweni Mwinuka ameeleza kuwa changamoto kubwa ya upungufu wa nguvu za kiume inachangiwa na lishe duni wanayotumia wanaume pamoja na kuwa na wapenzi wengi.

Mwinuka amesema hayo Mjini Kibaha wakati akifafanua kuhusu tatizo hilo ambapo ameeleza kuwa  wanandoa wanapaswa kuzingatia lishe bora katika milo yao, vilevile kwa vijana na hata watu wazima na kuacha tabia ya kuwa na wapenzi wengi wakati lishe ikiwa duni hivyo kushindwa kuwamudu.

Aina ya moshi unaotoka kwenye gari lako na unachoashiria

“Tunasisitiza lishe kuanzia inapotungwa mimba, mtoto anapotengenezwa yaani siku 1,000 hadi mtoto atakapofikisha miaka miwili, kwani suala hilo linaanzia kwenye ubongo,” amesema Mwinuka.

Ameongeza “pia kuna ugonjwa wa kisukari nao unachangia tatizo hilo, hivyo watu wanapaswa kwenda hospitali badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapatiwe matibabu, wakati mwingine ni msongo wa mawazo tu hakuna haja ya kutumia dawa bali ni ushauri tu.”

Aidha, amewashauri watu kuzingatia lishe na kula vyakula vya kujenga mwili, milo kamili ikiwa ni pamoja na ulaji wa matunda na  kuachana na uvutaji sigara.

Chanzo: Habari Leo