WASHINDI 100 WA MTOKO WA KIBINGWA NA BETIKA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO

0
49

WASHINDI 100 wa Kampeni ya mtoko wa kibingwa kupitia kampuni ya Betika wawasili rasmi Jijini Dar es salaam kushuhudia derby ya Kariakoo kesho.

Akizungumza na Wanahabari wakati wa Mapokezi ya washindi wa mtoko wa kibingwa  Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Betika  Nelson Pius amesema kuwasili kwa washindi hao kunaleta historia ndani a msimu huo wa 5 kutimiza washindi 100 kutoka mikoa mbalimbali huku Mshindi mmoja akiwa Mwanamke kutoka Chamazi Jijini Dar es salaam.

“Tayari washindi wetu wamewasili kutoka mikoani ikiwemo Geita,Mtwara,Sumbawanga, Simiyu,Songwe Dar es salaam na sehemu mbalimbali ni furaha yetu kuwa watakwenda kutazama derby ya Kariakoo kama dhamira ya kampuni ya betika ilivyoandaa shughuli hii tangu kuzinduliwa kwa Kampeni awali mwezi Febuari.”

Hata hivyo Pius ameeleza kuwa Washindi hao wamepatikana kupitia droo za kila siku ambapo mshiriki aliweza kuweka ubashiri wake kwa dau la shilingi mia 500.

“Tayari washindi wetu wametuwa dar mapema hivyo kutafatiwa na bata la mtoko wa kibingwa itakayofanyika kidimbwi huku siku ya kesho watasindikizwa na king’ora hadi uwanjani na watapata huduma ya kipekee.”

Kwa upande wake Mshindi kutoka Simiyu Bahame balele amesema amefurahi kufika Dar es salaam kwa usafiri wa mwewe huku akiongeza kuwa hakuwahi kupanda ndege hivyo kampuni ya Betika imetimiza ndoto hiyo aliyokuwa akiiota kila siku.

Huku akisisitiza kuwa derby hiyo anategemea kupata ushindi kwa timu yake ya Yanga.

Send this to a friend